06/04/2026
SAA YA KUJARIBIWA IKO TAYARI KUUJILIA ULIMWENGU WOTE ILI KUWAJARIBU WAKAAO JUU YA NCHI
“Kwa kuwa umelishika neno la subira yangu, mimi nami nitakulinda, utoke katika saa ya kujaribiwa iliyo tayari kuujilia ulimwengu wote, kuwajaribu wakaao juu ya nchi” (Ufunuo 3:10).
Katika mstari wetu wa ufunguzi, Yesu mwenyewe amesema hapo, iko “saa ya kujaribiwa iliyo tayari kuujilia ulimwengu wote, kuwajaribu wakaao juu ya nchi.” K**a saa hiyo ipo na inakuja ya kujaribiwa kwa wakaao juu ya nchi, maana yake ni kwamba tunatakiwa kujiandaa kwa ajili ya kujaribiwa katika wakati huo.
Kusudi la kujaribiwa kwa watu wote ni ili kupima imani za watu k**a ni za kweli, na kuona k**a tunaweza kuvumilia mpaka mwisho pasipo kumkana Yesu na pasipo kutenda dhambi yeyote, na kusafishwa ili tuweze kuwa wakamilifu na watimilifu bila kupungukiwa na neno lolote. Neno linasema;
“Amri hii ninayokuamuru leo mtaishika kuitenda, mpate kuishi na kuongezeka, na kuingia katika nchi ile ambayo BWANA aliwaapia baba zenu; nanyi mtaimiliki. Nawe utaikumbuka njia ile yote BWANA, Mungu wako aliyokuongoza…..katika jangwa (wakati wa kujaribiwa), ili akutweze, kukujaribu kuyajua yaliyo moyoni mwako, kwamba utashika amri zake, au sivyo. Akakutweza, akakuacha uone njaa, akakulisha kwa mana, usiyoijua wewe wala baba zako hawakuijua; apate kukujulisha ya kuwa mwanadamu haishi kwa mkate tu, bali huishi kwa kila litokalo katika kinywa cha BWANA.
Mavazi yako hayakuchakaa, wala mguu wako haukuvimba, miaka hiyo arobaini. Nawe fikiri moyoni mwako, ya kuwa k**a vile baba amrudivyo mwanawe, ndivyo BWANA, Mungu wako, akurudivyo. Nawe uzishike amri za BWANA, Mungu wako, upate kwenda katika njia zake, na kumcha. Kwa kuwa BWANA, Mungu wako, yuakuingiza katika nchi nzuri, nchi yenye vijito vya maji, na chemchemi, na visima, vibubujikavyo katika mabonde na milima; nchi ya ngano na shayiri, na mizabibu, na mitini, na mikomamanga; nchi ya mizeituni yenye mafuta, na asali;
nchi utakayokula mikate humo, pasina shida, hutapungukiwa na kitu ndani yake; nchi ambayo mawe yake ni chuma, na milima yake yafukuka shaba. Nawe utakula ushibe, utamshukuru BWANA, Mungu wako, kwa nchi nzuri aliyokupa. Jihadhari, usije ukamsahau BWANA, Mungu wako, kwa kutozishika amri zake, na hukumu zake, na sheria zake, ninazokuamuru leo” (Kumbukumbu 8:1-11).
“Nami nitalileta fungu lile la tatu na kulipitisha kati ya moto, nami nitawasafisha k**a fedha isafishwavyo, nami nitawajaribu k**a dhahabu ijaribiwavyo; wataliitia jina langu, nami nitawasikia; mimi nitasema, Watu hawa ndio wangu; nao watasema, BWANA ndiye Mungu wangu” (Zacharia 13:9).
“Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali; mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi. Saburi na iwe na kazi kamilifu, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu bila kupungukiwa na neno” (Yakobo 1:2-4).
“Wala si hivyo tu, ila na mfurahi katika dhiki pia; mkijua ya kuwa dhiki, kazi yake ni kuleta saburi; na kazi ya saburi ni uthabiti wa moyo; na kazi ya uthabiti wa moyo ni tumaini; na tumaini halitahayarishi; kwa maana pendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu tuliyepewa sisi” (Warumi 5:3-5).
“Maana mnahitaji saburi, ili kwamba mkiisha kuyafanya mapenzi ya Mungu mpate ile ahadi. Kwa kuwa bado kitambo kidogo sana, Yeye ajaye atakuja, wala hatakawia. Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani; Naye akisita-sita, roho yangu haina furaha naye. Lakini sisi hatumo miongoni mwao wasitao na kupotea, bali tumo miongoni mwa hao walio na imani ya kutuokoa roho zetu” (Waebrania 10:36-39).
“Wakifanya imara roho za wanafunzi na kuwaonya wakae katika ile Imani, na ya kwamba imetupasa kuingia katika ufalme wa Mungu kwa njia ya dhiki nyingi” (Matendo 14:22).
“K**a tukistahimili, tutamiliki pamoja naye; K**a tukimkana yeye, yeye naye atatukana sisi; K**a sisi hatuamini, yeye hudumu wa kuaminiwa. Kwa maana hawezi kujikana mwenyewe” (2 Timotheo 2:12-13).
“Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili” (1 Wakoritho 10:13).
“Wapenzi, msione kuwa ni ajabu ule msiba ulio kati yenu, unaowapata k**a moto ili kuwajaribu, kana kwamba ni kitu kigeni kiwapatacho. Lakini k**a mnavyoyashiriki mateso ya Kristo, furahini; ili na katika ufunuo wa utukufu wake mfurahi kwa shangwe. Mkilaumiwa kwa ajili ya jina la Kristo ni heri yenu; kwa kuwa Roho wa utukufu na wa Mungu anawakalia. Maana mtu wa kwenu asiteswe k**a mwuaji, au mwivi, au mtenda mabaya, au k**a mtu ajishughulishaye na mambo ya watu wengine.
Lakini ikiwa kwa sababu ni Mkristo asione haya, bali amtukuze Mungu katika jina hilo. Kwa maana wakati umefika wa hukumu kuanza katika nyumba ya Mungu; na ikianza kwetu sisi, mwisho wao wasioitii injili ya Mungu utakuwaje? Na mwenye haki akiokoka kwa shida, yule asiyemcha Mungu na mwenye dhambi ataonekana wapi? Basi wao wateswao kwa mapenzi ya Mungu na wamwekee amana roho zao, katika kutenda mema, k**a kwa Muumba mwaminifu” (1 Petro 4:12-19).
“Lakini yeye aijua njia niendeayo; Akisha kunijaribu, nitatoka k**a dhahabu. Mguu wangu umeshik**ana sana na hatua zake; Njia yake nimeishika, wala sikukengeuka. Sikurudi nyuma kuiacha amri ya midomo yake; Nimeyatunza maneno ya kinywa chake zaidi ya riziki yangu” (Ayubu 23:10-12).
“Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa msh*taki wenu Ibilisi, k**a simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze. Nanyi mpingeni huyo, mkiwa thabiti katika imani, mkijua ya kuwa mateso yale yale yanatimizwa kwa ndugu zenu walioko duniani. Na Mungu wa neema yote, aliyewaita kuingia katika utukufu wake wa milele katika Kristo, mkiisha kuteswa kwa muda kidogo, yeye mwenyewe atawatengeneza, na kuwathibitisha, na kuwatia nguvu” (1 Petro 5:8-10). Amina!!