Kingdom of Heaven Ministry - Dr. Jacob & Devota Makaya

Kingdom of Heaven Ministry - Dr. Jacob & Devota Makaya Make the Kingdom of God your #1 priority and the King will provide everything you need (Mat 6:33)

01/01/2026

Happy New Year 2026 people of God. May the grace of God be with you all.

Love & Blessings

07/06/2025

BEWARE OF POLITICAL MINISTERS

Believers- beware of “political ministers.” These are ministers who seek self-glory using the political system. Because of their “political position,” it limits what they can or cannot say in the pulpits. They certainly won’t stand up like John the Baptist or OT prophets who confronted wicked leaders.

When wicked leaders are surrounded by false prophets, we should certain expect the same outcome as what we read in the Bible during the times of kings.

Ministers need to teach believers to be obedient to God and to obedient to authorities within biblical parameters. However, when ministers start to become political, it reveals something deeper about them. God warned them already, and now He is exposing them. (I sincerely hope these ministers repent before it gets to this point.)

If it gets to the point where these political ministers are no longer above the reproach, it means they no longer have biblical qualifications to lead God’s people, and the Holy Spirit will depart from them (assuming the Holy Spirit was upon them to begin with.) These ministers will have gone “the way of Balaam.”

REMEMBER: God will never compromise His truth for any political reason. So when you see ministers do that, it is a sign they have departed from the truth.

SAD TRUTH: It is sad when unbelivers can easily disern that these political ministers are cons but many believers, who are supposed to be led by the Holy Spirit, cannot see it. May God have mercy.

12/09/2024

MAOMBI YA REHEMA KWA AJILI YA TANZANIA – SEHEMU YA PILI

Namshukuru Mungu ambaye anipa neema ya kuandaa post hii ya pili, kwani ni muendelezo wa ile ya kwanza, ili sisi k**a kanisa tuzidi kuendelea kuomba rehema za Mungu juu ya Tanzania.

Kuna ujumbe ambao Mungu aliuleta kwa nyakati tofauti kusudi tuzidi kuomba, lakini pia kujiandaa k**a kanisa kwa yale ambayo hayana budi kutokea hapo baadae.

April 11, 2020: (Huu ni ujumbe niliutuma mwaka 2020 ambao hivi karibuni nimekuwa nikiletewa kuutafakari na kuomba juu ya Tanzania.)

Nilionyeshwa ndotoni nipo mahali pamoja na aliyekuwa raisi wa Tanzania, Magufuli. Magufuli akasema kuwa ameota ndoto ya kuwa mguu wake mmoja una vidole 7. Wale watu aliokuwa akiwaambia na kuwaonyesha mguu wake hawakumuelewa.

Ndipo (nikiwa ndotoni) nikamwambia Magufuli na kusema maneno haya: “vidole 7 maana raisi wa 7 wa Tanzania atakuwa mpinga Kristo ambaye atakwenda kulipiga vita kanisa la kweli la Kristo.”

Baada ya kumwambia maneno hayo alianza kuongea mambo kadhaa juu ya Tanzania (ambayo siwezi kutaja). Ndipo akaondoka na kukawa na watu wengi waliotaka kupiga naye picha.

(kwa context yetu, picha ni kwa ajili ya kumbukumbu. Ujumbe ulikuwa unamaanisha kwamba ipo siku watanzania watamkumbuka Magufuli).

Nilishtuka katika ile ndoto natetemeka na usingizi ukaondoka. Ieleweke kuwa naposema huyo kiongozi atakuwa mpinga Kristo, haina maana huyo ndiye yule mnyama wa Ufunuo 13. Wapinga Kristo wapo wengi na roho ya mpinga Kristo hata sasa inafanya kazi.

Kiongozi huyo hataleta vita dhidi ya madhehebu, bali vita yake italenga kanisa la kweli, k**a jinsi ambavyo mfalme Herode alifanya.

Neno linasema, “Panapo majira yale yale Herode mfalme akanyosha mikono kuwatenda mabaya [baadhi] ya watu wa kanisa. Akamwua Yakobo, ndugu yake Yohana, kwa upanga” (Matendo 12:1—2).

Nyakati zitafika ambapo watu watakuwa wanafungwa gerezani, kuuawa, au kuzuiliwa kuihubiri injili ya kweli kwa uhuru. Kutakuwa na mfumo ambapo ujasiri wa kusimama na kukemea maovu ya viongozi utakuwa haupo au ni mgumu.

Yohana Mbatizaji alipomkemea Herode kwa sababu ya uovu wake, ilimgharimu maisha yake.

Yezebeli alitumia nafasi ya mumewe mfalme Ahabu kuleta vita dhidi ya Nabii Eliya. Mkewe Herode alitumia nafasi ya mumewe kumuua Yohana Mbatizaji.

Hivyo ujasiri wa kanisa kusimama na kukemea maovu yanayotendwa katika nchi utazidi kupungua. Kuna nchi ya Africa ambayo utekaji na watu wasio na hatia na kuuawa ni jambo la kawaida, ila hutasikia sana kanisa linakemea uovu huo.

Ndio maana kanisa linatakiwa kuwa makini pale ambapo viongozi wasio wafuasi wa Kristo wanaposhiriki katika “ujenzi wa kanisa.” Kuna pesa au ushirikiano unaolenga kuuwa vitu kanisani.

Wale ambao wanafahamu upinzani wa ujenzi wa hekalu wakati wa Ezra (Soma Ezra 4) wanaweza kuelewa maana ya neno hilo.

Siku kadhaa zilizopita, nilikuwa nafakari ule ujumbe juu ya raisi wa 7 wa Tanzania sana. Ndipo nikaongozwa kusoma zaidi juu ya wafalme wa 7 wa na Israeli na Yuda baada ya ufalme kugawanyika (ukiacha yule Zimri ambaye aliyetawala siku 7).

Baada ya ufalme kugawanyika, kiongozi wa 7 wa Israeli alikuwa Ahabu na mkewe alikuwa Yezebeli. Ahabu na Yezebeli walibahatika kuwa mtoto wa k**e aliyeitwa Athalia.

Athalia alikuwa mbaya zaidi ya Yezebeli kwani alikusudia kuua uzao wote wa wafalme (2 Wafalme 11). Lakini pia malakia Athalia ndiye mtawala wa 7 wa Yuda.

Athalia alikuwa mwanamke wa kwanza na wa pekee kutawala Yuda ambaye hakuwa kabila la Yuda. Athalia aliingia madarakani baada ya aliyekuwa mfalme wa Yuda Ahazia (aliyetawala mwaka mmoja) “kufariki.” Athalia alitawala Yuda kwa miaka 6.

Ujumbe wa hapa chini sikukusudia kuutoa, ila Mungu ameweka msukumo wa kuutoa pamoja na tarehe ambazo nilipata kwani kuna mambo yanataka kufanana na yale yaliyotokea Israeli na Yuda.

March 13, 2021: Usiku huu nilionyeshwa mambo matatu ambayo pia yaliweka msukumo wa kuzidi kuomba rehema juu ya Tanzania. (Tarehe 13 ilikuwa siku 6 kabla ya kuapishwa raisi wa 6 wa Tanzania ambaye aliingia madarakani katika mwaka wa 6 wa kutawala kwake Magufuli.)

Sehemu ya kwanza: Nilisikia sauti inasema “Magufuli is dead (Magufuli amefariki)” ambayo iliambatana na roho ya huzuni nyingi moyoni.

Sehemu ya pili: Nilionyeshwa mtu ambaye nilimtambua vizuri kwani mara nyingi Magufuli alipokuwepo, naye alikuwepo. Nikamuona mtu huyo akikanyaga kichwa cha mtu (mtanzania). Kichwa kile kilipondeka kabisa na kuwa k**a chapati, na hakuweza kuinuka.

Sehemu ya tatu: Nilionyeshwa gari jeupe ambalo kwa nje lilionekana ni zuri. Ila ndani gari lile lilikuwa chafu na limejaa vumbi kila mahali. Gari lile lilikuwa linaenda usiku kwenye barabara mbaya ya vumbi. Taa za gari lile zilikuwa na mwanga hafifu ambao haukufika mbali.

Mungu aliachilia neema ya kuelewa. Sehemu ya tatu ilikuwa inazungumzia muelekeo ambao nchi itakwenda kupitia. Matukio hayo matatu yalifuatana kwa mfululizo huo. Ndio maana kanisa linahitaji sana kuomba juu ya Tanzania.

March 19, 2021: Niliona maono ambapo Ziwa Tanganyika lilikuwa limekauka lote na hamna maji. Ndani ya ziwa kwa chini nikaona udongo na samaki 2, mmoja mdogo mwingine mkubwa kidogo, ambao walionekana wakaribia kufa.

(Kitabu cha Ufunuo na Isaya vinatuonyesha kuwa mito/bahari kukaushwa vinazungumzia juu ya “hukumu ya Mungu.”

March 19, 2021 ni tarehe muhimu Tanzania kwani ni siku ambayo Samia aliapishwa kuwa raisi wa sita Tanzania. Samia ni raisi wa kwanza Tanzania ambaye alizaliwa Zanzibar.

Samia alikuwa raisi baada ya raisi Magufuli “kufariki” ndani ya mwaka wa kwanza wa kutawala kipindi cha pili, ikiwa ni mwaka wa sita wa kutawala kwake Magufuli nchini Tanzania.

(Endelea kuomba rehema za Mungu juu ya Tanzania na viongozi wake ili watawale katika haki. Lengo la ujumbe huu ni ili kuzidi kuomba rehema za Mungu juu ya nchi ya Tanzania na kuzidi kuombea viongozi. Mungu wetu ni mwingi wa rehema.

Katika sehemu ya kwanza, tumeona kuwa kuna mambo kiongozi wa nchi akifanya, ghadhabu ya Mungu ipo siku itashuka katika taifa au ufalme.

Pia endelea kuombea uchaguzi wa viongozi wa nchi utakaofanyika October 2025. Kumbuka kuwa maombi ya watakatifu yanaweza kupelekea Mungu kuinua viongozi bora au kuwatumia wale walioko madakarani ili watende mapenzi ya Mungu na kusimamia haki.

Ubarikiwe,

Jacob M.

12/09/2024

MAOMBI YA REHEMA KWA AJILI YA TANZANIA – SEHEMU YA KWANZA

Amani ya Mungu Baba wateule wa Mungu. Natumaini Mungu mnaendelea vizuri. Namshukuru sana Mungu kwa neema yake, na kibali hiki kuandika post hii ili tuweze kuelewa umuhimu wa kuomba kwa ajili ya nchi.

Post hii nimeigawa katika sehemu mbili ambazo zinategemea ili kuelewa vizuri.

Sehemu ya kwanza: Inalenga kuweka msingi wa kibiblia kuhusu viongozi ambao Mungu anawainua katika taifa, na umuhimu kwa kuwaombea ili watende mapenzi ya Mungu.

Sehemu ya pili: Inalenga juu ujumbe wa Tanzania ili watu tuzidi kuelewa njia za Mungu na kuzidi kuomba rehema za Mungu juu ya nchi ya Tanzania.

UMUHIMU WA KUOMBEA VIONGOZI

Biblia inatufundisha kuwa kuna mambo yanayotokea katika mataifa ambayo huwa ni matokeo na mambo yanayoendelea katika ulimwengu wa roho.

Nehemia 3-4 zinatuonyesha upinzani uliokuwepo katika ujenzi wa hekalu kwa jinsi ya mwili.
Zakaria 3 inaonyesha upinzani kutoka kwa Shetani katika ulimwengu wa roho na jinsi ulivyoathili mambo yanayoendelea katika nchi.

Neno la Mungu linatuonyesha kuwa kuna wafalme na wakuu wa falme katika ulimwengu wa roho waliopo juu ya mataifa. Kumbuka kuwa Shetani ndiye “mfalme wa uwezo wa anga” (Waefeso 2:2).

Danieli alipokuwa katika kwa muda wa majuma matatu, alionyeshwa kitu kilichokuwa kinaendelea katika ulimwengu wa roho.

“Lakini [mkuu wa ufalme Uajemi] alinipinga siku ishirini na moja; bali, tazama, huyo Mikaeli, mmoja wa hao wakuu wa mbele, akaja kunisaidia; nami nikamwacha huko pamoja na [wafalme] wa Uajemi” (Danieli 10:13). Ukiendelea kusoma, Danieli aliambiwa:

“Ndipo akasema, Je! Unajua sababu hata nikakujia? Na sasa nitarudi ili nipigane na mkuu wa Uajemi; nami nitakapotoka huku, tazama, [mkuu wa Uyunani] atakuja” (Danieli 10:20).

Unaweza kusoma Danieli 10 yote ili kuelewa habari ile katika context, ila nilitaka uone hawa waotajwa: “mkuu wa ufalme wa Uajemi,” “wafalme wa Uajemi,” na “mkuu wa Uyunani” ni wafalme waliopo katika ulimwengu wa roho juu ya mataifa, siyo watu.

Wafalme hawa wanaweza kutumia viongozi katika taifa au ufalme ili wafanye mambo yaliyo kinyume na mpenzi ya Mungu. Tuangalie mfano:

1 Nyakati 21:1—2

1 Tena Shetani akasimama juu ya Israeli, akamshawishi Daudi kuwahesabu Israeli.

2 Basi Daudi akamwambia Yoabu, na wakuu wa watu, Nendeni kawahesabu Israeli toka Beer-sheba mpaka Dani; mkanipashe habari, nipate kujua jumla yao.

Ukiendelea kusoma habari hii, Mungu alimkasirikia mfalme Daudi kwa kile kitendo cha kuwahesabu watu. Pamoja na kwamba watu wake wa karibu walimshauri asifanye, tayari Shetani alishaweka jambo hilo ndani ya moyo wa Daudi ili alifanye.

Ndipo tunaona Mungu akimtuma nabii Gadi, aliyekuwa muonaji wa Daudi, kwenda kwa mfalme Daudi.

1 Nyakati 21:11—14

11 Basi Gadi akamwendea Daudi, akamwambia, Bwana asema hivi, Kubali upendavyo;

12 miaka mitatu ya njaa; au miezi mitatu kuangamia mbele ya adui zako, ukipatwa na upanga wa watesi wako; au siku tatu upanga wa Bwana, yaani tauni katika nchi, na malaika wa Bwana akiharibu kati ya mipaka yote ya Israeli. Haya ufikiri ni jawabu gani nimrudishie yeye aliyenituma.

13 Naye Daudi akamwambia Gadi, Nimeingia katika mashaka sana; basi sasa na nianguke katika mkono wa Bwana; kwa kuwa rehema zake ni nyingi sana; wala nisianguke katika mkono wa mwanadamu.

14 Basi Bwana akawaletea Israeli tauni; nao wakaanguka wa Israeli watu sabini elfu.

Nimekupa maandiko haya ili uone kuwa kitendo cha mfalme Daudi kuamua kuwahesabu watu alipata ushawishi kutoka kwa Shetani. Lakini Mungu aliadhibu taifa la Israeli na watu elfu 70 walikufa ndani ya siku 3.

Hivyo kiongozi anaweza kufanya maamuzi ya aina fulani, na Mungu akaadhibu taifa (utaelewa maana ya hili katika sehemu ya pili juu ya maono ya Mungu juu ya Ziwa Tanganyika).

Tuone mfano mwingine ambapo mambo yaliyokuwa yanatokea chini yaliathiriwa na yale yanayotokea katika ulimwengu wa roho.

Joshua na Israeli walipokuwa wakipigana na Waamaleki, neno la Mungu linasema, “Ikawa, Musa alipoinua mkono wake, Israeli walishinda; na alipoushusha mkono wake, Amaleki walishinda” (Kutoka 17:11).

Ukiendelea kusoma utaona kuwa ilibidi mikono ya Musa iwe imeinuliwa mpaka Israeli walipowaangamiza maadui. “Kuinua mikono” pia ni lugha ya kibiblia ambayo inazungumzia kuomba (1 Timotheo 2:8).

Waefeso 6 pia inatuambia juu ya falme na mamlaka, wakuu wa giza, na majeshi ya mapepo ambavyo vinatumiwa na Shetani kupinga kusudi la Mungu (Waefeso 6:12—20) hasa inapohubiriwa “injili ya amani.”

Falme wa mamlaka hizi za giza huwa zinawatumia pia watu, hasa walio na mamlaka katika maeneo au nchi, k**a tulivyoona mfano kwa mfalme Daudi.

Kwa sababu hiyo, ni muhimu kuwaombea walioko kwenye mamlaka ili maamuzi yao yatokane (yawe influenced) na maombi ya watakatifu. Viongozi wasipokuwa influenced kwa maombi wanaweza kuwa influenced na upande wa giza.

(Ndio maana kuna viwango vya kuruhusu nchi zingine ziwe na mamlaka katika maeneo ya nchi kiuhalali ambayo yanafungua malango ya kiroho na kumpa Shetani uhalali wa kufanya mambo yake katika taifa hilo. Naamini unaelewa ninachozungumza.)

Hivyo kanisa linatakiwa pia kuomba sana kwa ajili ya viongozi walioko kwenye mamlaka, hata k**a kwa jinsi ya mwili kuna mambo wanayafanya ambayo hatuyapendi au hatukubaliani nao.

Nakumbuka mwaka 2020 Mungu alipokuwa akisema juu ya Joe Biden kwenda kuchaguliwa raisi wa Marekani, kuna mambo mengi Mungu alikuwa akionyesha juu ya nchi. Naamini Mungu alikuwa anayaleta ili nisimame katika nafasi na kuomba.

Usiku mmoja nilionyeshwa mkono wa mtu wa kushoto upo k**a umeoza. Mungu alifunua kuwa hiyo inazungumzia juu ya “uovu” ambao Democratic Party watafanya. Marekani, “kushoto” ni Democratic Party na “kulia” ni Republican Party.

Kwenye Biblia, moja ya tafsiri ya mkono wa kushoto ni “utajiri” na “heshima” hapa duniani.

“Ana wingu wa siku katika mkono wake wa kuume, Utajiri na heshima katika mkono wake wa kushoto” (Methali 3:16). (Sasa unaweza kuelewa kwa nini utawala wa Biden uliharibu hayo maeneo mawili.)

(Kuna watu ambao wanaweza kuelewa kwa nini wamekuwa wakionyeshwa adui akiwinda sana mikono yao ndotoni au katika maono). Kinachowindwa siyo mikono kwa jinsi ya mwili bali kile ambacho mtu amebeba.)

Hii iliweka msukumo wa kuomba rehema juu ya Marekani na kuwaombea viongozi pia kwani nilijua maamuzi wanayofanya yanatuathiri sote. Hivyo, wakati wote, tunatakiwa kuomba kwa ajili ya viongozi wa nchi ili Mungu ndiye awatumie kwa ajili ya kusudi lake.

(Kumbuka Mungu kumtumia kiongozi kwa ajili ya kusudi lake na kiongozi huyo kutembea na Mungu ni vitu viwili tofauti.) Tunaposoma vitabu vya Wafalme na Mambo ya Nyakati, tunaona viongozi wa aina mbili:

Viongozi waliofanya “mema machoni pa Bwana.”
Viongozi waliofanya “mabaya machoni pa Bwana.”

Viongozi wanapofanya mema machoni pa Bwana, kunakuwa na utawala wa haki katika nchi, na mkono wa Mungu unakuwa pamoja na kiongozi huyo. Mfalme Hezekia alifanya yaliyo mema machoni pa Bwana na neno linasema, kila alikokwenda alifanikiwa (2 Wafalme 18).

Kiongozi anapofanya mema na kuwa mnyenyekevu mbele za Mungu, mkono wa Mungu unakuwa pamoja naye na pia unakuwa juu ya nchi.

Kiongozi anapofanya mabaya machoni pa Bwana, Mungu anaweza kuleta mabaya juu ya kiongozi huyo au akaleta mabaya juu ya nchi. Ahabu alipotenda maovu mbele za Bwana, Mungu
alimuinua Yehu kwa ili kuiangamiza nyumba ya Ahabu.

Mfalme Manase alitenda maovu sana kiasi kwamba Mungu akamtumia mfalme wa Ashuru kumfunga Manase na kumpeleka Babeli. Mfalme Manase alimpolilia Mungu, Mungu wa rehema, alimrehemu na kumrudisha katika ufalme wake (2 Nyakati 33).

Pamoja na kwamba Mungu alimsamehe Manase, uovu alioufanya ulikuwa mkubwa mno kiasi kwamba ghadhabu ya Mungu ilikuwa lazima ije kwa Yuda. Kuna kiwango cha uovu ambapo kiongozi anapoufanya, ghadhabu ya Mungu lazima ishuke katika taifa.

Yeremia 15:1—4

1 Ndipo Bwana akaniambia, hata wangesimama mbele zangu Musa na Samweli, moyo wangu usingewaelekea watu hawa; watupe, watoke mbele za macho yangu, wakaende zao.

2 Kisha itakuwa watakapokuambia, Tutoke, tuende wapi? Utaawaambia, Bwana asema hivi, Walioandikiwa kufa, watakwenda kufa; au kufa kwa upanga, watakufa kwa upanga; au kufa kwa njaa, watakufa kwa njaa, au kutwekwa nyara, watakuwa mateka.

3 Nami nitaamrisha juu yao namna nne, asema Bwana; upanga uue, na mbwa wararue, na ndege wa angani, na wanyama wakali wa nchi, wale na kuangamiza.

4 Nami nitawafanya kuwa kitu cha kutisha katika falme zote za dunia, [kwa sababu ya Manase], mwana wa Hezekia mfalme wa Yuda, kwa sababu ya mambo aliyoyatenda katika Yerusalemu.

Nilitaka uone kuwa pamoja na kwamba mfalme Manase alitubu mbele za Mungu na Mungu alimsamehe, tunaona bado Mungu aliadhibu taifa kwa sababu ya makosa yake.

Kiongozi anaposimama katika haki na kutenda yaliyo mema mbele za Mungu, au watu wa Mungu wanapoomba na kuutafuta uso wa Mungu juu ya nchi, Mungu ambaye ni mwingi wa rehema anaweza “kuchelewesha” mabaya aliyoyakusidia.

Mfalme Yosia ni mfalme ambae alienenda mbele za Mungu vizuri. Wakati wa utawala wake, Mungu hakuleta mabaya ila baada ya Yosia ndipo Mungu akayaleta yale mabaya. (Soma 2 Wafalme 22—23 juu ya Yosia).

2 Wafalme 23:25—26

25 Kabla ya huyo, hapakuwa na mfalme mfano wake, aliyemwelekea Bwana kwa moyo wake wote, na kwa roho yake yote, na kwa nguvu zake zote, sawasawa na sheria zote za Musa; wala baada yake hakuinuka mmoja mfano wake yeye.

26 Walakini Bwana hakuuacha ukali wa ghadhabu yake nyingi ambayo hasira yake iliwaka juu ya Yuda, kwa sababu ya machukizo yote ambayo Manase amemchukiza.

Nimekupa mifano hiyo michache ili uweze kuelewa nyakati za rehema au hukumu ya Mungu kwa kuangalia aina ya viongozi ambao Mungu anaowainua katika taifa.

Mungu huwa anainua viongozi wa aina mbili: kiongozi ambaye nchi inamuhitaji au kiongozi ambaye nchi inamstahili kwani wakati mwingine kiongozi ni taswira ya nchi.

Kwa mfano: Raisi wa 5 wa Tanzania ni Magufuli. Pamoja na kwamba watu wanaweza kuwa na mitazamo tofauti, Tanzania ilimuhitaji yule kiongozi na siku zitakuja ambapo Tanzania watamkumbuka huyu kiongozi (utaelewa katika sehemu ya pili).

Pia Mungu anaweza kuinua kiongozi ambaye nchi inamstahili.

Kwa mfano: Mungu alimuinua Joe Biden kwa nyakati hizi kwani nchi ilistahili kutokana na uovu unaoendelea. Maovu ya Sodoma na harakati nyingi za utoaji mimba, na mengine ni taswira ya mahali ambapo nchi ilipo.

Haya ni makosa ambayo ghadhabu ya Mungu itakuja juu ya taifa la Marekani, hata k**a siyo sasa. Dhambi za Manase ndiyo zilipelekea ghadhabu ya Mungu kushuka katika Yuda.

Pia ni muhimu kuelewa njia za Mungu kwani tunaona kuwa Manase ambaye alikuwa mmoja wa wafalme waovu ndiye aliyetawala Yuda miaka mingi kuliko wafalme wote (alitawala miaka 55).

(Pia kumbuka kuwa Manase alizaliwa kile kipindi ambacho Hezekia aliongezewa miaka 15 ya kuishi wakati nabii Isaya alipokuwa ametumwa na Mungu kumwambia Hezekia kuwa atakufa)

Nimekupa msingi kwa ufupi ili kuelewa umuhimu wa kuomba rehema za Mungu na kuomba kwa ajili ya nchi na viongozi. Mambo tunayosoma kwenye Biblia juu yanatufundisha sana jinsi Mungu anavyoshughulika na nchi katika nyakati zetu. Unaweza kuelewa katika post inayofuata.

Wenu katika Kristo Yesu,
Jacob M.

12/01/2024

Amani ya Mungu Baba na Bwana watu Yesu Kristo iwe pamoja nanyi!

Namshukuru sana Mungu kwa neema yake ambayo ametupatia, hasa katika kuzidi kumjua Yeye kupitia maandiko yake matakatifu. Natumaini wanafunzi wa Kristo mnaendelea vizuri.

Pamoja na kwamba sikupata neema ya kufundisha neno lake kwa muda, tumekuwa pamoja, nikiwakumbuka katika maombi yangu pia. Nawashukuru pia kwa wale mmekuwa mkiomba kwa ajili yangu pia.

Naamini kuwa mambo yale ambayo Mungu amekuwa akinifundisha tutapata fursa ya kujifunza kwa pamoja ili sote tuzidi kukua katika kumjua Mungu kupitia Kristo Yesu. Sote tu wanafunzi wa Kristo, na Mungu ametupa karama tofauti kwa ajili ya kuuimarisha mwili wa Kristo.

Pia namshukuru Mungu sana kwa wale ambao wamekuwa na mzigo wa kuomba kwa ajili ya nchi ya Tanzania. Ni maombi yangu kuwa Mungu atazidi kuweka mzigo ndani ya mioyo ya watu kusimama na kuiombea nchi ya Tanzania.

(Tunaposoma vitabu vya Wafalme na Mambo ya Nyakati juu ya wafalme wa Israel na Yuda, inatupa kuelewa rehema ya Mungu au hukumu ya Mungu kwa kuangalia aina ya viongozi ambao Mungu aliwainua kwa nyakati tofauti na makusudi tofauti.)

Kuna ujumbe wa Mungu kwa ajili ya Tanzania ambao nitautuma siku hizi za karibuni. Sehemu ya kwanza nilituma mwaka 2020. Naamini Mungu anatukumbusha ili kanisa lizidi kuomba, lakini pia tuzidi kujiandaa kwa ajili ya mambo ambayo hayana budi kutokea nchini.

Namshukuru sana Mungu ambaye ameachilia neema ya kuzidi kujifunza zaidi neno lake, na anakwenda kuendelea kutufundisha kwa namna ya tofauti. Neno la Mungu ndiyo mwongozo wetu tunaomwamini Kristo kwani ni taa ya miguu yetu.

Pia namshukuru Mungu kwa ajili ya wale ambao Mungu amekuwa akiwatumia kwa ajili ya kuwaombea watoto. Kazi mnayofanya ni njema mbele za Mungu. Mungu azidi kuwapa nguvu katika jambo hili.

Mwenyezi Mungu azidi kuwalinda na kuwapigania, hasa katika kipindi hiki tunapoenda kumaliza mwaka na kuanzia mwaka mwingine.

Neema ya Mungu izidi kuwa pamoja nanyi, na Mwenyezi Mungu azidi kuwapa roho ya upendo, hekima, na ufunuo katika kumjua Yeye.

Wenu katika Kristo,
Jacob M.

04/15/2024

ZAKA KATIKA AGANO JIPYA: BIBLIA INASEMAJE?

Bwana Yesu apewe,

Mmoja wa wanafunzi wa Kristo aliuliza swali juu ya zaka katika Agano Jipya. Nimepata msukumo kulijibu hili swali katika upana ili kumsaidia ye yote aliye na swali k**a hili.

ZAKA KABLA YA AGANO LA KALE: Kuna maeneo mawili ambapo tunaona zaka hata kabla ya Agano la Kale.

ZAKA YA IBRAHIMU KWA MELKIZEDEKI: Neno linatuambia kuwa baada ya Abramu kupata habari kuwa ndugu yake alitekwa na adui, Abramu alitumwa watumishi waendele kuwakomboa. Alipokutana na Melkizedeki, Abram alimpa fungu la kumi la vitu vyote (Mwanzo 14:20).

Zaka ambayo Abramu aliitoa kwa Melkizedeki ilikuwa hiari, na siyo k**a sheria kwani hapa hakukuwa na sheria. Mtu akiamua kutoa zaka k**a Abramu anaweza kufanya kwa hiari.

NADHIRI YA ZAKA YA YAKOBO: Yakobo aliota ndoto ambapo Mungu alimpa ahadi ambazo Mungu alimpa Ibrahimu na uzao wake. Ndipo Yakobo akaweka nadhiri kutoa zaka.

Mwanzo 28:20—2

20 Yakobo akaweka nadhiri akisema, Mungu akiwa pamoja nami akinilinda katika njia niiendeayo, na kunipa chakula nile, na nguo nivae;

21 nami nikirudi kwa amani nyumbani kwa baba yangu, ndipo Bwana atakuwa Mungu wangu.

22 Na jiwe nililolisimamisha k**a nguzo litakuwa nyumba ya Mungu; na katika kila utakalonipa hakika nitakutolea wewe sehemu ya kumi.

Yakobo aliweka nadhiri ya kuwa Mungu akimbariki na kumpa mahitaji yake na kurudi kwa amani nyumbani kwa baba yake, ndipo atampa Mungu fungu la kumi.

Katika Agano Jipya, mtu anaweza kuweka nadhiri ya zaka k**a Yakobo kuwa Mungu akimtendea mambo fulani katika maisha yake atampa fungu la kumi.

K**a umeweka nadhiri ya kumtolea Mungu halafu usitoe, hapo itakuwa dhambi. Biblia inasema, bora usiweke nadhiri kuliko kuweka na kutokufanya (Kumbukumbu 23:21—22).

ZAKA KATIKA AGANO LA KALE

Katika Agano la Kale, kutoa zaka ilikuwa ni sheria (yaani ni lazima). Mungu aliagiza zaka ziendele katika maeneo makubwa matatu:

1. ZAKA YA MAONGEO KWA AJILI YA KULA MBELE ZA BWANA KILA MWAKA:

Zaka hii ilitolewa mara moja kwa mwaka. Zaka hii Mungu aliagiza mtoaji aile yeye na nyumba yake.

Kukumbuku 14:22—26

22 Usiache kutoa zaka ya kumi katika maongeo yote ya mbegu zako, yatokayo shamba mwaka baada ya mwaka.

23 Nawe utakula mbele za Bwana, Mungu wako, mahali atakapochagua apakalishe jina lake, zaka ya nafaka zako, na divai yako, na mafuta yako, na wazaliwa wa kwanza wa makundi yako ya ng’ombe na ya kondoo; ili upate kujifunza kumcha Bwana, Mungu wako, daima.

24 Na njia ikiwa ndefu mno nawe, usiweze kuzichukua kwa kuwa mahali ni mbali mno atakapochagua Bwana, Mungu wako, apakalishe jina lake, hapo atakapokubarikia Bwana, Mungu wako,;

25 ndipo uzibadili ziwe fedha, na kufunga zile fedha uende nazo mkononi mwako, hata mahali atakapochagua Bwana, Mungu wako,

26 na zile fedha zitumie kwa cho chote itakachotamani roho yako, ng’ombe, au kondoo, au divai, au kileo, au roho yako itakacho kwako cho chote; nawe utakula mbele za Bwana, Mungu wako; tena furahi, wewe na nyumba yako.

Zaka hii watu walitoa ili wale mahali ambapo Mungu kaweka jina lake. Kusudi la zaka hii tunaliona mwisho wa msitari wa 23. Zaka hii ilikuwa mara moja kwa mwaka.

Katika Agano Jipya, hii zaka hatukuagizwa kwani hatuoni maeneo maalumu ambayo Mungu anayaweka jina lake. Jerusalemu pekee ndipo Biblia inasema Mungu ameweka jina lake milele (2 Nyakati 33:7).

Kwenye Agano Jipya hatuambiwi kwenda Jerusalemu kila mwaka kula zaka hii na familia zetu. Hii ilikuwa katika Agano la Kale.

2. ZAKA KWA MGENI, MJANE, YATIMA, NA MLAWI KILA BAADA YA MIAKA MITATU:

Kuna zaka ambayo Mungu alikusudia itolewe kwa mgeni, mjane, yatima, na kabila la walawi. Zaka hii ilikuwa inatolewa kila baada ya miaka mitatu.

Kumbukumbu 14: 27—29

27 na Mlawi aliye ndani ya malango yako usimwache, kwani hana fungu wala urithi pamoja nawe.

28 Kila mwaka wa tatu, mwisho wake, toa fungu la kumi lote la maongeo yako ya mwaka huo, uliweke ndani ya malango yako.

29 na Mlawi kwa kuwa hana fungu wala urithi Pamoja nawe, na mgeni, na yatima, na mjane aliyefiwa na mumewe, walio ndani ya malango yako, na waje wale; na kushiba; ili kwamba Bwana, Mungu wako, akubarikie katika kazi yote ya mkono wako uifanyayo.

KWA WALAWI: Moja ya makusudi ya Mungu kuwapa kabila la Walawi zaka ni kwa sababu “wao hawakuwa na fungu wala urithi” (Hesabu 18:21—24). Katika Agano Jipya, zaka kwa ajili ya kabila la Walawi hatukuagizwa.

KWA MJANE NA YATIMA: Katika Agano Jipya, Mungu hakuweka sheria ya kutoa zaka kwa ajili ya mjane/yatima.

Katika Agano Jipya hatujaagizwa kutoa zaka kwa yatima, wageni, na wajane. Ila ni mapenzi kabisa hawa hatu katika jamii wasaidiwe kwa kadri mtu unavyoliwa. Hivyo mtu anaweza kutoa zaka au zaidi kwa hiari kwa ajili ya kuwasaidia wahitaji.

3. ZAKA KWA AJILI YA UKUHANI KWENYE HEKALU (ZAKA YA ZAKA).

Kuna zaka ambayo walawi walikuwa wanaitoa kwa kuhani mkuu. Kusudi la zaka hii ilikuwa kwa wale wanaofanya utumishi wa ukuhani katika nyumba ya Mungu.

Zaka hii inaitwa “zaka ya zaka” kwa sababu ni zaka iliyokuwa inatolewa katika zaka ambayo Walawi wameipokea.

Nehemia 10:38—39

38 Naye kuhani, mwana wa Haruni, atakuwako pamoja na Walawi, watwaapo zaka Walawi; nao Walawi wataipandisha [zaka na hiyo zaka] nyumbani mwa Mungu wetu, vyumbani, katika nyumba ya hazina.

39 Kwa kuwa wana wa Israeli na wana wa Lawi wataleta sadaka ya kuinuliwa ya nafaka, na mvinyo, na mafuta, vyumbani, kwa kuwa ndimo vilimo vyombo vya patakatifu, na makuhani watumikao, na mabawabu, na waimbaji; wala sisi tatutaiacha nyumba ya Mungu wetu.

Nimeweka msisitizo katika [zaka ya hiyo zaka] kwani hii ni zaka ambayo Walawi waliagizwa kuitoa kwa ajili ya utumishi katika hekalu Yerusalemu. Zaka hii ndiyo iliyotajwa katika Malaki 3:10 ambayo Walawi walikuwa wanaiba.

Malaki 3:8—10

8 Je! Mwanadamu atamwibia Mungu? Lakini ninyi mnaniibia mimi. Lakini ninyi mwasema, Tumekuibia kwa namna gani? Mnebiibia zaka na dhabihu.

9 Ninyi mmelaaniwa kwa laana; maana mnaniibia mimi, naam, [taifa hili lote.]

10 Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema Bwana wa majeshi; mjue k**a sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwageni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.

Mungu alisema kuwa makuhani Walawi na kabila yote ya Lawi wasiwe na urithi kwani Mungu ndiye urithi wao. Wao waliagizwa kula sadaka zinazotolewa (Kumbukumbu 18:1—2), hii ni pamoja na zaka k**a tumevyoona hapo juu.

Katika zaka ya Walawi, nao Walawi walitakiwa kutoa zaka katika zaka kwa kuhani mkuu kwa ajili ya watumishi katika nyumba ya Bwana, yaani [makuhani, mabawabu, na waimbaji].

Hivyo ukisoma context ya aina ya zaka ya Malaki 3:10 utaona kuwa hii ni zaka iliyotakiwa kutolewa na Walawi, yaani fungu la kumi la ile zaka ambayo wao wameipokea kwa watu.

Walawi walikuwa wanapokea zaka, lakini wao hawakuwa wanatoa “zaka ya hiyo zaka” kwa ajili ya watumishi watumikao katika nyumba ya Mungu. Ndio maana Mungu anasema walikuwa wanaiba.

Walikuwa wanaiba kwa sababu Walawi walipokea zaka, ila wao hawakuwa wanatoa. Ndio maana laana ilienda kwa taifa lote. Wale waliokuwa wanaiba walisababisha Mungu kulaani taifa lote la Israel.

Zaka ya zaka ndiyo ina baraka iliyotajwa katika Malaki 3:10b: “mjue k**a sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwageni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.”

ZAKA YA ZAKA KATIKA AGANO JIPYA: Zaka ya zaka iliyotajwa katika Nehemia 10:38 na Malaki 3:10 kanisa halikupewa hii sheria kuitoa kwani ule ukuhani wa Walawi hekaluni haupo. Hivyo baraka ya Malaki 3:10b siyo kwa ajili ya kanisa.

“Nyumba yangu” ambayo imetajwa katika Malaki 3:10 siyo “mahali wanapokutanika kuabudu” katika Agano Jipya. Mtu akitoa zaka kwa hiari kwa ajili watumishi wanaotumika kanisani haina shida, ila hii siyo sheria katika Agano Jipya.

ZAKA KATIKA AGANO JIPYA (YAANI BAADA YA KUFUFUKA KWA YESU)

Kwenye Agano Jipya, Mungu hakuweka utoaji zaka k**a sheria. Agano Jipya limesisitiza juu ya “kutoa kwa moyo,” yaani kwa kadri mtu unavyoamua ndani ya moyo wako. Kwenye Agano la Kale, kutoa zaka ilikuwa ni sheria, siyo hiari.

Na tunaona kuwa zaka ambayo Walawi wahakutoa kwa ajili ya nyumba ya Mungu ndio ilileta laana. Zaka ya wajane/yatima, au ile ya kila mwaka siyo iliyoleta laana kwa taifa.

Mitume walipoagiza “mambo ya lazima” kwa watu wamataifa, kuishika torati haikuwa mojawapo na hii ilimpendeza Roho Mtakatifu, yaani ilimpendeza Mungu (Matendo 15).

Bwana Yesu alipokuwa anawahubiria wale waliokuwa chini ya torati, alizungumza na Mafarisayo alisemea:

“Lakini, ole wenu, Mafarisayo, kwa kuwa mwatoa zaka za mnanaa na mchicha na kila mboga, na huku mwaacha mambo ya adili, na upendo wa Mungu; iliwapasa kuyafanya hayo kwanza, bila kuyaacha hayo ya pili” (Luka 11:42). Pia soma Mathayo 23:23.

Bwana Yesu alisema kuwa Mafarisayo walikuwa “wapenda pesa” (Luka 16:14). Hivyo unaweza kuelewa kwa nini waliweka mkazo katika utoaji sadaka, ila mambo ya muhimu zaidi k**a upendo kwa Mungu, waliyaacha.

Bwana Yesu alikuwa anaongea na watu ambao wako chini ya sheria ya Musa na aliagiza watoe zaka, kutoa sadaka ya kutakaswa kwa aliyekuwa na ukoma (Marko 1:40—44), na sadaka za “madhabahuni” zilizopo katika torari (Mathayo 5:23—25).

Baada ya kufufuka kwa Yesu Kristo, yaani katika Agano Jipya, mitume hawakuagiza utoaji zaka, sadaka za kutakaswa, au sadaka zingine katika madhahabu hekaluni.

Katika Agano Jipya, sadaka ambayo Mungu ameiamuru ni kwa ajili ya wale ambao wanapeleka injili. Neno linasema, wanaopolekea injili wanastahili posho/ujira (Mathayo 10:10; Luka 10:7; 1 Timotheo 5:17—18). Mtume paulo pia aliandika, na kusema,

“Hamjui ya kuwa wale wazifanyao kazi za hekalu hula katika vitu vya hekalu, na wale waihudumiayo madhabahu huwa na fungu lao katika vitu vya madhabahu?Na Bwana vivyo hivyo ameamuru kwamba wale wauhubirio Injili wapate riziki kwa hiyo Injili” (1 Wakorintho 9:13—14).

Hivyo ni amri ya Mungu kwa watu wake kutoa kwa ajili ya wale wanaopeleka injili. Kwa matajiri na wale ambao Mungu amewawezesha kipesa, neno linasema, kutoa na kushirikiana na wengine kwa moyo (1 Timotheo 6:8—9). Hii siyo amri.

Katika Agano Jipya, hakuna andiko ambalo linazungumza juu ya utoaji zaka k**a sheria. Mtu anaweza kutoa zaka kwa hiari na akapeleka anapoongozwa, ila siyo sheria.

Kila anayefundisha zaka k**a sheria kwa kanisa lazima atumie maandiko ya Agano la Kale tun a context ya Malaki 3:8—10 lazima ibadilishwe ili “nyumba ya Mungu” iwe “kanisa” na “makuhani Walawi” wawe watumishi kanisani. Hili siyo fundisho la mitume.

Ila kwa wale ambao Mungu amekujalia, ni mapenzi ya Mungu 100% kutoa kwa moyo. K**a ni kusaidia wenye shida, kutoa zaka ya hiari, kutoa kwa watumishi, yote haya yanampendeza Mungu yakifanywa kwa moyo safi.

Ila kutoa kwa wainjilisti kupeleka injili, hii siyo hiari, bali ni amri kutoka kwa Mungu.

Ubarikiwe,

Jacob Makaya

Address

Atlanta, GA

Telephone

+18064452050

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Kingdom of Heaven Ministry - Dr. Jacob & Devota Makaya posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Kingdom of Heaven Ministry - Dr. Jacob & Devota Makaya:

Share