22/10/2025
KIKI ZA MLAANIWA MWAKIPESILE NA MKEWE.
Kuanzia wiki iliyopita nilikuwa makini nikifuatilia habari ya Mwakipesile kutoroka mbeya na kukimbilia kusikojulikana, ambako yeye anasema yuko mafichoni, japo hajaweka wazi kuwa yuko ndani ya nchi au nje, chanzo cha kuondoka Mbeya anasema ni suala la kiusalama, anasema anafuatiliwa na watu wasiojulikana, alijigamba kwa kusema "hata mkewe hajui alipo" Hatujakaa sawa mara jana tena nimepata habari kuwa Mkewe pia ametoroka kwa sababu zile zile za mumewe, nae anadai anafuatiliwa!!
kwanza mnatakiwa mjue, Mimi sijaanza kufuatilia mienendo ya kikosi kazi leo, nilianza miaka mingi sana k**a miaka 4 au 5 nyuma, nikawa nawachunguza sana mienendo yao baada ya kuwa wanajigamba sana kuwa wao ndio Watakatifu pekee hapa Duniani, madhehebu na dini zingine na wachungaji wengine wote ni Takataka, ndio maana mahubiri yao mara nyingi ni ya kushambulia Wachungaji wa Makanisa mengine, na wote ambao sio sehemu ya kikosi kazi, kila mahubiri ya makanisa mengine lazima wayakosoe, lakini wao hata wakihubiri utumbo basi wanashangilia na kujiona wako sawa kwa kila kitu.
ok, tunarudi kwenye mada, hiyo ni intro tu kwa wageni wa page hii.
MWAKIPESILE hayuko mafichoni, yuko kule kule mbeya, amefichwa na vijana wake wa kikosi kazi, lengo la kutangaza hii taharuki na kupost kwamba Wamekimbia nchi na wako mafichoni ni muendelezo wa Chuki zake kwa serikali, na ni katika harakati za kuendelea kuwajaza chuki wananchi dhidi ya serikali kwasababu yeye ana chuki na serikali kwasababu Serikali imegomea usajili wa kanisa lake la Kigaidi na kisiasa.
naam, kanisa lake limejaa harakati za kidunia na sio injili, harakati hizo za kidunia ni pamoja na SIASA na MASIMANGO na KICHAMBUA MAISHA YA WENGINE, hawahubiri injili ya WOKOVU.
Kwahiyo msitahayarike na huyu Mtu, sasahivi anatapatapa tu, maana wameshagombana pia na Mpambe wake maarufu ambae ni PASCHAL CASSIAN 😂
Hizi ni Drama ti na kiki ili aendelee kuongelewa, hakuna mchungaji hapo, ni MBWA-MWITU mpenda KIKI na kubweka