02/07/2020
NJIA 10 ZA KUWEKA AKIBA (SAVING OPTIONS) ZENYE KUFUATA MASHARTI YA KIISLAM (Sharia compliant).
By Salum Awadh, SSC Capital.
Ni vugumu kufanikiwa kifedha (financial success) na kuwa huru kifedha (financial freedom), k**a hatuwezi;
- Kukuza vipato
- Kuweka akiba
- Kuwekeza akiba zetu
Njia zipo nyingi, ila ni muhimu kujua ni njia zipi zinakubalika kisharia, na hii ni muhimu kwa wote mjasiriamali na mwajiriwa;.
1. Kuweka akiba ya muda mrefu
- Hii ni muhimu k**a una malengo ya muda fulani ujao na huna hakika k**a utakuwa na fedha katika kipindi hicho. Utafanya hivyo kwa kufungua akaunti ya benki kwa kipindi maalum (fixed deposit) yenye tija pia ya kupata gawio la faida. Tembelea benki za kiislam k**a Amana, KCB, NBC, na PBZ kwa maelezo zaidi.
2. Kuwa na bima
Sheria ya kiislam imeweka utaratibu wa bima ya kiislam k**a kinga ya majanga ambayo yanaweza kutokea na wewe kushindwa kuyamudu kwa kukosa akiba muda huo. Utaratibu wa bima ya kiislam unaitwa Takaful, na utaanza muda c mrefu nchini Tanzania, fuatilia taarifa hizi kwa karibu ili uweze kujiunga
3. Wekeza akiba yako
Zipi njia nyingi zinazokubalika kisharia kuwekeza akiba yako bila wewe kufanya kazi ya uzalishaji wa faida ya shughuli husika (Passive investments). Njia hizi ni pamoja na kununua hisa (shares), kuwekeza kwenye masoko ya mitaji ya mikopo (bonds), au kuwekeza kwa njia ya mifumo ya kununua vipande (unit trusts). Uislam pia umeweka utaratibu wa aina za hisa za kununua (sharia complaint shares/stocks), Sukuk (islamic bonds), na sharia compliant mutual funds. Hizi kwa Tanzania hamna kwa sasa, ila unaweza kununua kwenye nchi nyingine k**a Malaysia, Dubai, Bahrain, UAE, n.k, unaweza kutumia kampuni ya Wahed kwa ku download app yao na kujisajili
4. Kununua bidhaa za thamani k**a vile dhahabu na silver, na ku*iweka. Na bdae ku*iuza unapohitaji fedha kwa mahitaji yako. Omba ushauri zaidi kwa wataalam wa sharia kwenye hili.
5. Kufungua akaunti za malengo. Huu ni utaratibu wa mabenki ambao unakusaidia kufungua akaunti maalum kwa malengo maalum k**a vile malengo ya kwenda hajj, akaunti za watoto kuandaa ada za shule, n.k
6. Kujiunga na mifuko ya kijamii (social security schemes). Hii inakusaidia kuwa na akiba ya kukuwezesha kukidhi mahitaji kipindi ambacho huwezi kuwa na chanzo kingine cha mapato, k**a vile ukistaafu, ukipata ulemavu wa kudumu, au kufikwa na mauti na wategemezi wako kuendelea kupata mahitaji yao. Upo utaratibu wa kisharia juu ya mifumo hii, ongea na wataalum wa sharia kukushauri zaidi kabla ya kujiunga.
7. Kutengeneza mfuko wa familia wa waqf ( Family trust)/ ( Al-waqf al-’ahli).
Kwa utaratibu huu unaweza kusajili waqf na kuweka kiasi cha fedha ambacho kinaweza kuwanufaisha wategemezi wako. Mfuko huu unakuwa unasimamiwa na mtaalam (Trustee/mutawalli), ambaye atawajibika kuutunza, kuukuza, na kukidhi mahitaji ya wategemezi yatakoidhinishwa na mtoaji (Waqif)
8. Kuwekeza kwenye mifumo ya umiliki wa pamoja wa majengo (Real estate investment trusts (REITs).
Huu ni utaratibu ambao unanunua hisa kwenye kampuni ya real estate iliyoanzishwa maalum kwa ajili ya kuwekeza kwenye majengo (real estate), kampuni inasimamiwa na mtaalam, na kila mwisho wa mwaka faida inayotokana na kipato cha kodi, kinagawiwa wanahisa k**a gawio (dividend), unaweza kufanya hivi pia kwa kuwekeza kwa njia ya crowdfunding inayojihusisha na miradi ya ujenzi tu k**a vile ethiscrowd.com iliyopo singapore, inayozingatia sheria ya kiislam.
9. Kujiunga na utaratibu wa vyama vya kuweka na kukopa (saccos) au benki za kijamii (Village community banks(VICOBA). Hii ni nzuri zaidi kwenye vipato vidogo. Hakikisha kabla hujajiunga kuwa chama hicho kinaendeshwa kwa misingi ya kiislam ikiwemo kutotoza riba katika miamala yake.
10. Usiweke fedha kwenye kibubu. Watu wengi wamekuwa na tabia ya kuweka fedha kwenye kibubu, hii si njia salama na si njia bora kuweka akiba. Hali hatarishi (risks) zipo nyingi k**a vile kuibiwa, kushika moto, kuingia maji, kupata tamaa ya kukivunja, na pesa kutoweza kuwekwa kwenye njia mbadala ambazo utaweza kuweka akiba na utapata faida.
HITIMISHO
Ili uweze kufanikiwa katika haya, hakikisha;
1: unasoma majarida ya mifumo ya fedha na uwekezaji wa kiislam mara kwa mara
2. Omba ushauri kwa wataalum wa fedha na uwekezaji
3. Omba ushauri kwa wataalum wa sharia ( sharia scholars)
4. Hudhuria mafunzo na makongamano
5. Jifunze elimu ya bajeti, vipato, na matumizi
6. Jitahidi kuishi chini ya kipato chako ili uweze kubaki na akiba
7. Jua tofauti ya majitaji na matakwa ( needs and wants)
8. Fahamu kuwa akiba yako na kipato chako kitalizimika kutolewa zaka, pale ambapo zikikidhi masharti na viwango. Pata ushauri kwa wataaalm wa sharia